Wenye magari watapata afueni mwezi huu baada ya mafuta ya petroli na diesel kupungua kwa mujibu wa tathmini mpya iliyotangazwa na tume ya Petroli na kawi . lita moja ya petrol hapa jijini itauzwa kwa shilingi 108 Nukta 05 kutoka shilingi 112 na senti 81 .lita moja ya disel itauzwa kwa shilingi 101 na senti 96 kutoka bei ya awali ya shilingi 103 nukta 03 . bei ya mafuta taa hata hivyo imepanda hadi shiingi 101 nukta 08 kutoka shilingi 100 na senti 64 .
Bunge la Kaunti ya Busia ndilo la hivi punde kuukata mswada wa punguza mizigo uliopendekezwa na chama cha Thirdway Alliance .waakilishi wa kaunti wamesema wananchi hawakuhusishwa katika kutayarisha mswada huo na vile vile utarejesha nyuma hatua zilizoafikiwa kufanikisha ugatuzi .
Chuo kikuu cha Moi Kimewafurusha viongozi watano wa wanafunzi ambao wanadaiwa kupanga maandamano yaliokumbwa na ghasia wiki jana na kusababisha chuo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana . naibu chansella Isaac Kosgey amethibitisha kwamba wanafunzi hawatakubaliwa kurejea shuleni humo .
Mahakama moja mjini Voi imempata na hatia mwanamume mwenye umri wa miaka 56 aliyembaka bintiye mwenye umri wa miaka 17.Mwemba Gereza anadaiwa kutekeleza kitendo hicho Agosti 28 mwaka 2016 katika eneo la Buguta huko Voi.Hakimu mkaazi wa Voi Fredric Nyakundi amesema upande wa mashtaka ulidhibitisha kuwa mshukiwa alitekeleza kitendo hicho cha kinyama
Chama cha ODM kimetakiwa kuwahakikishia wakenya kwamba kitadumisha amani wakati wa uchaguzi mdogo wa kibra .mbunge wa kiharu Ndindi Nyoro amesema kisa kama kilichotokea mwishoni mwa wiki ambapo msafara wa mgombeaji wa Jubilee Mcdonald mariga ulishambuliwa kwa mawe sio jambo linalofaa kukubaliwa .
Serikali itazidisha mara dufu jitihada za kukabiliana na udanganyifu katika mitihani ya kitaifa mwaka huu .afisa mkuu mtendaji wa baraza la kitaifa la mihani Mercy Karogo amewashauri maafisa wakuu wa elimu katika kaunti ndogo kuhakikisha kwamba wanafuatilia kikamilifu usimamizi wa zoezi la mtihani katika maeneo yao .