Aibu! MCA wa Kiambu akamatwa kwa kuunda vyeti bandia

Bwana Robert Kibe Githango, MCA wa mtaa wa Kiamangi kaunti ya Kiambu anatakiwa kufika mbele ya mahakama ya Milimani jumatano.

Bwana Robert Kibe alitiwa mbaroni na maafisa wa EACC kwa madai ya kuwapa vyeti bandia vya masomo.

Vilevile, Githongo atahukumiwa kwa makosa manne ikiwemo kupeana habari za uongo, kutengeneza vyeti bandia, kuzungumzia vyyeti bandia na kunena mambo ya uongo.

Kikundi cha Anti-corrruption kilianza utafiti wa kesi hiyo na kujua kuwa, MCA huyu alikuwa ametengeneza vyeti bandia ili aweze kupata uhuru wa kuanza masomo katika chuo kikuu cha Jomo Kenyatta.

Amini usiamini,Githongo alitengeneza vyeti bandia ili aweze kuanza masomo ya Diploma akizaingatia masomo ya Uongozi.