MAHAKAMA kuu imekataa kutoa agizo la kuziruhusu serikali za kaunti kununua dawa kutoka kwa wauzaji wengine wa dawa isipokuwa shirika la dawa nchini KEMSA .JAJI WELDON Korir amelikabidhi suala hilo kwa jaji mkuu atajayetaja jopo la majaji wa kuisikiliza na kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo . kesi hiyo inapinga uamuzi wa kulitaka shirika la KEMSA kuwa pekee linaloziuzia kaunti dawa .
Halmashauri ya utunzi wa mazingira nchini NEMA imeagizwa kutekeleza notisi ya kuyafunga maeneo ya burudani ya Kiza, B club na Space Lounge mtaani Kilimani baada ya wakaazi kulalamikia kuchezwa kwa muziki wa sauti ya juu katika sehemu hizo za burudani .
Matayarisho ya mtihani wa KCPE yanakamilishwa hivi leo kote nchini kabla ya mtihani huo kuanza hapo kesho ,.huko North rift usalama umeimarishwa katika vituo vyote vya kuanyia mtihani hasa katika sehemu ambazo huathiriwa na visa vya wizi wa mifugo
IWAPO Mgonjwa wa kansa anaamua kukueleza masaibu anayopitia akiugua ni vyema kusikiliza badala ya kulinganisha hali yake na yako au ya mtu mwengine . mtaalam wa kansa Philip Odiyo amesema kulinganisha hali ya mgonjwa mmoja hadi mwingine sio jambo la busara kwani kila mmoja ana vitu tofauti alivyopitia .
Rais Donald Trump wa marekani ametangaza kwamba kiongozi aliyekuwa akijificha wa kundi la Islamic State , Abu Bakr al Baghdadi alijiuwa mwenyewe wakati wa uvamizi wa kikosi maalum cha Marekani nchini Syria. Katika tangazo la runinga , bwana Trump alitangaza kwamba gaidi huyo nambari moja duniani amefariki wakati wa uvamizi hatari wa usiku kaskazini magharibi mwa Syria na vikosi maalum vya Marekani.