Maeneo bunge 40 yanakadiriwa kuvunjwa baada ya Sensa 2019

Tume ya IEBC italazimika kuvunja maeneo bunge zaidi ya 40 kwa kukosa kutimiza idadi ya watu inayotakikana baada ya matokeo ya sensa 2019.

Kulingana na takwimu za sensa 2019, maeneo bunge 40 yaliyo na idadi ya watu chini ya 114,889  yanafaa kufutiliwa mbali kulingana na ripoti ya nwenyeketi wa tume huru ya kutathmini mipaka na maeneo Andrew Ligal.

Hata hivyo, baadhi ya maeneo bunge 27 hayakuvunjwa 2009 licha ya kutotimiza idadi ya watu hitajika ya kati ya 93,196.6 na 79,882.8.

Tume ya IEBC ikiongozwa na Wafula Chebukati inapanga kutathmini upya mipaka kulingana na idadi ya watu kabla ya uchaguzi wa 2022.

Ifuatayo ni baadhi ya maeneo bunge yanayokadiriwa kuvunjwa na mipaka yake kuratibiwa upya:

Lamu East (22,258), Mwatate (81,659), Kuria East (96,872), Budalangi (85,977), Mt Elgon (78,873) na Laikipia North(36,184).

Mengine ni Tiaty (73,424), Keiyo North (99,176), Marakwet East (97,041), Samburu North (67,391), Samburu East (77,994), Pokot South (80,661), Turakana North (65,218), Loima (107,795), Kangema(80,447), Tetu (80,453), Mathioya (92,814), Mkurwe-in (89,137), Kang'undo (97,917), Mwingi East (85,139), Eldas (88,509), Lafey (83,457) na Kathiani (111,890).

Mbunge wa Naivasha Jayne Kihara alisema kwamba maeneo bunge yenye idadi kubwa sana ya watu yanafaa kuongezewa fedha nyingi za CDF ili kuhakikisha usawa wa ugavi wa raslimali hiyo.

"Mgao wa CDF unakandamiza maeneo bunge yaliyo na idadi kubwa ya watu kwa kuwa maeneo yote yanapewa mgao sawa wa fedha hizo," alisema.