Mke mwema hutoka kwa Mungu!
Mwanahabari Waihiga Mwaura alibarikiwa sana na Maulana kwa kupata mke mwema.Yaani mke mwenye mapenzi tele.
Joyce Omondi ni mke amchaye Mungu sana, yeye huweka Mungu mbele na kumtumainia kwani anaelewa fika kuwa,wahenga waligonga ndipo waliposema,Mungu hamuachi mja wake.
Mumewe, Waihiga Mwaura amepanda ngazi katika taaluma yake ya uanahabari kwenye runinga ya Citizen TV. Mwaura amekabidhiwa usukani kuendesha gurudumu la Hussein Mohamed aliyeondoka na sasa atakuwa akiongoza taarifa za siku ya Jumanne usiku.
Baada ya ujumbe huu wa kufurahisha moyo kuibuka, Joyce Omondi alichukua fursa hii kumpongeza mumewe.
Kupitia mtandao wa kijamii, Joyce aliandika, ni makuu yale ambayo Mungu anaweza kufanya katika maisha yako unapojitolea kumtumikia.