+ Picha) Mshukiwa wa mauaji ya Tob Cohen ashtakiwa wizi wa kimabavu Naivasha

Korti ya mjini Naivasha imemshtaki mfanyabiashara Peter Karanja kwa kosa la wizi wa kimabavu.

Karanja ni mshukiwa katika kesi linalomuusisha na mauaji dhalimu ya Tob Cohen.

Jamaa huyu alikuwa mpenzi wa mbunge wa Gilgil Martha Wangari.

Mshukiwa huyu anadaiwa kuwapora walinzi wawili kwa kutumia nguvu.

Inadaiwa kuwa yeye, kakake Joel Kuria na Peter Maina walivamia boma la mbunge huyu lililopo Gilgil na kuwajeruhi na kuwaibia walinzi.

Stakabadhi za korti zinaonyesha kuwa Novemba 9, watatu hawa walivamia eneo la Teachers Estate , Gilgil huku wamejihami kwa silaha za vita.

Waliiba simu na pesa za Eric Nyogesa na John Kamau.

Katika mahakama hiyo ya Naivasha, watatu wawili waliwakilishwa na wakili Mburu.

Baadaye walikana mashtaka hayo.

Kesi yao ilichukua mkondo tofauti wakati walinzi waliojeruhiwa waliamua kuwasamehe na kuondoa mashtaka dhidi yao.

Wakili Mburu alihoji kuwa walinzi hao walikuwa radhi kuondoa kesi baada ya kuwasamehe nje ya mahakama.

Aidha, upande wa mashtaka uliamua kuondoa kesi hiyo sio sawa kwani huenda walinzi hao walitishiwa kuafikia uamuzi huo.