Picha ya siku: Kutana na familia ya msanii wa Mugithi Samidoh

Samidoh (1)
Samidoh (1)
Samuel Muchoki almaarufu, 'Samidoh' ni mmojawapo wa wasanii ambao 'wamelipuka' au waliokuwa midomoni mwa wakenya wengi mwaka wa 2019.

Msanii huyu wa nyimbo za aina ya Mugithi, anajulikana kwa ustadi wake katika nyanja ya burudani haswa safu ya nyimbo za kikuyu na nyota yake imekuzidi kutamba mwaka huu.

Kile wengi hawajui kuhusu Samidoh ni kuwa yeye ni afisa wa polisitangia mwaka wa 2014 na mchana yeye huwa akifanya ulinzi huku jioni akiwatumbuiza maelfu ya mashabiki wake.

Samidoh anatambulika kwa nyimbo kama Ndiri mutwe mwega na murata wa ngai.

Kitu kimoja ambacho msanii huyu mkarimu na mnyenyekevu, anatambulika nacho ni kuwa huwa ameiweka familia yake kama siri na sio wengi wanaojua kuihusu.

Hata hivyo, leo katika pilkapilka za uchambuzi wa mitandao ya kijamii nilibahatika kukutana na picha za familia yake ambazo zilichapishwa na msanii na mcheshi, Henry Desagu wakiwa likizo Diani.

Kutokana kwa picha hizo, ni ishara tosha Samidoh ana bibi mrembo na wawili hao ni wazazi wa wana wawili, mmoja wa kike na mwingine wa kiume.

Tazama picha hizi.

https://www.instagram.com/p/B5DkUbiAqiR/