PATANISHO: Mke wangu alikula fedha za kununua shamba

Bernard aliyekosana na mkewe bi Claire, mwaka jana kisa na maana, fedha, ndiye aliyetuma ujumbe akiomba apatanishwe.
"Tulikuwa tunapanga kununua shamba lakini nilipata ametumia fedha zile karibu elfu sabini. Nilipofika nyumbani akanieleza kuwa atanirudishia zile fedha mwezi wa saba na nikarudi Nairobi."

Aliongeza,

Baada ya mda fulani alinipigia simu akisema hajapata fedha zile ila alikuwa na elfu hamsini lakini baadaye akaanza uwongo na hakurudisha zile fedha. Kwa hasira kuu nilimfukuza na hatujazungumza tangu hayo yatokee." 

Kulingana na Bernard ni kama mkewe alitumia zile fedha kwa upande wa mamake.

Wawili hao wamejaliwa na watoto watatu baada ya kuishi kwa ndoa ya miaka kumi.

Bernard alikiri kuwa wakati wa mwisho wawili hao kuzungumza ilikuwa mwezi wa kumi na akamfanyia shopping ya kupeleka kwa mamake. Hata hivyo anashuku kuwa mama mkwe ndiye anayemkalia mkewe ili asirudi kwake.

Tulipojaribu kumpigia Claire simu hakupatikana ila bi Mercy dadake mdogo ndiye aliyepokea simu. Kulingana na bi Mercy kuna fununu kuwa dadake atarudi kwa ndoa yake.

"Namuombea Claire arudi kwa ndoa kwani wana watoto na ningependa wawalee pamoja kwani anampenda Bernard sana." Alisema Mercy.

Ujumbe wa Bernard wa mwisho kwake mkewe ulikuwa,

Mimi sina ubaya naye na hakuna kitu nitamfanyia naoomba tu arudi kwa ndoa yake tuendelee na maisha."