Chris Martin na mastaa wawili zaidi kutoka Jamaica wawasili nchini

Staa mkubwa wa nyimbo za dancehall, Chris Martin amewasili nchini hii leo tayari kuwaburudisha wakenya siku ya jumamosi.

Chris Martin ambaye sio mara ya kwanza kutua na kuwatumbuiza humu nchini (mara ya mwisho alikuwa Kenya ilikuwa mwaka wa 201) aliwasili akiwa na magwiji wenzake; D Major na Future Fambo.

Martin anajulikana kwa nyimbo zake kama let her go, pirate of the carribean na weekend love. D Major pia anatambulika kwa nyimbo kama; That's What Loves About na Real know real.

Future fambo ambaye anapendewa sauti yake nzito anatambulika kwa nyimbo kama puff puff pass na rum and redbull.

Baada ya kulakiwa kwenye uwamja wa ndege wa JKIA na wanahabari, wasanii hao walizuru afisi za spika wa kaunti ya Nairobi, Beatrice Elachi.

Tazama picha zifuatazo.