Kidosho aliyeshukiwa kuvuruga penzi la Rayvanny na Fahyma aolewa

Video vixen wa ngoma ya I Love ya Rayvanny amefunga ndoa na mchumba wake wa kipindi kirefu.

Nana anatuhumiwa kuchepuka na staa wa muziki wa kizazi kipya Rayvanny.

Aidha, wawili hawa walipinga uvumi huu na kusema kuwa hawapo katika mahusiano ya kimapenzi.

Katika mahojiano na kituo cha habari nchini Tanzania, Nana alikana habari za kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na staa huyu.

"Tulipiga picha nyingi na hiyo ilikuwa sehemu ya kazi yangu. Mimi na Rayvanny ni marafiki. Hatuna mahusiano ya kimapenzi. Nipo kwenye uhusiano na mwanamume wangu na kila mtu anajua. Siwezi kufanya kufanya vituko vya kijinga hivi kwa sababu tumekuwa naye kwa miaka minne." Alisema Nana.

Rayvanny pia alijitetea na kusema kuwa Nana sio sababu ya kuachana na Fahyma.

“Sipo kwenye mahusiano na Nana, tena ana mahusiano yake ambayo nayaheshimu sana sana.Kichupa ni kizuri kwani kinaonyesha ukweli na mapenzi yapo. Nilitaka video hiyo iwe jinsi ilivyo..” alisema Rayvanny.

Taarifa za kuolewa kwa Nana kunadhibitisha kuwa tuhuma za Rayvanny kutoka kimapenzi na Nana zilikuwa za uongo.

" Ni rasmi mimi ni mkewe, Alhamdululah," Nana aliandika Insta.