Ulianza kuimiliki lini Kenya, Ruto amuuliza Raila Odinga

ruto
ruto
Naibu rais William Ruto ametaka kujua nafasi ya kinara wa Raila Odinga katika serikali ya Jubilee.

Hii ni baada ya Odinga kuonekana katika mstari wa kwanza kutoa mwelekeo wa ripoti ya BBI.

Raila amenukuliwa katika vyombo vya habari akisema kuwa wananchi wanapaswa wawe watulivu wakati huu ripoti ya BBI inapigwa msasa na jopo kazi lililoteuliwa.

https://twitter.com/WilliamsRuto/status/1210650282767589382

Tamko la Raila linaonekana kumkera naibu wa rais ambaye amehoji kuwa kiongozi huyu hana mamlaka ya kuwaagiza wakenya kuhusu jinsi wanavyotakiwa kufanya.

"Kenya imekuwa kitu kimoja tangu zamani. Ulianza kuimiliki lini hadi sasa unatuagiza kuwa watulivu, hadi utuamulie kinachotufaa!" alisema katika ukurasa wake wa Twitter.