Woga wa kuwa mpweke na kutojua hali ya mkewe imembidi atafute msaada wa Gidi na Ghost.
Kelvin ametuma ujumbe katika kipindi kinachoruka asubuhi katika kituo hiki akitaka usaidizi.
Ruth ni mke wa pili na ana mimba ya miezi 8.
"Aliniomba pesa ya kuenda kliniki nikamwambia sina. Nashindwa shida iko wapi? Hatuishi pamoja na nilikuwa nategemea sana uhusiano wake baada ya bibi yule mwingine kuwa mashida kidogo katika uhusiao wetu. Nilikuwa nadhani nimefika mahali nilikuwa nataka...." Alisimulia Kelvin.
https://www.instagram.com/p/B6H92ZUgZbI/
Wawili hawa wameishi katika uhusiano wa miaka 2.
Gidi amekubalia ombi lake na kumpigia simu.
"Si mimi niliharibu kazi yako. Tafuta vile utaangalia majukumu yako..." Amesema Ruth.
Katika mawasiliano ya wawili hawa, ni dhahiri kuwa Kelvin kukosa kazi kulichangia wao kukosa.