Arifa hiyo ya gazeti rasmi la serikali sasa inatoa fursa kwa jopo hilo la wanachama 14 kuifanyia marekebisho ripoti ya mwanzo iliyokuwa imetolewa kwa umma . Washirika wa Ruto hata hivyo wanashuku kwamba rais na Bwana Odinga wana hila dhidi ya Ruto na wanalenga kuitumia ripoti hiyo a BBI kumzuia naibu wa rais Kumrithi rais Kenyatta baada ya uchaguzi wa 2022 .
Wanachama wa jopo kazi hilo ni seneta wa Garissa Yusuf Haji, Askofu Lawi Imathiu, Maison Leshomo, James Matundura, Rose Museu, Agnes Kavindu and Saeed Mwaguni. Wengine ni Askofu Peter Njenga askofu mkuu Zaccheaus Okoth, Adams Oloo, Seneta Amos Wako, Florence Omose, Morompi Ronkei na John Seii. Makatibu wa pamoja wa jopo hilo ni Martin Kimani na Paul Mwangi. Kamati hiyo itawakabidhi rais na bwana Odinga ripoti yake Kufikia Juni tarehe 30.