'Vera ndiye alinitongoza, sikuwa namtaka,' Otile Brown

Huu waweza kuwa mwaka mpya lakini kwa waliokuwa wapenzi, Otile Brown na Vera Sidika, uhondo unaozunguka maisha yao bado wazidi kupamba moto.

Hii ni baada ya msanii Otile Brown katika mahojiano ya moja na runinga ya Wasafi msanii huyu alifichua kuwa Vera Sidika ndiye aliyemtongoza ila sio yeye.

Alisema,

VERA NI FRENEMY WANGU, SINA TATIZO NAE, NILIKUWA NAFANYA VIZURI KABLA YA VERA, WATU HAWAJUHI SIJAWAHI KUMTONGOZA, ALINITAFUTA MWENYEWE, ALIKUWA ANANIPIGIA SANA SIMU NA WALA NILIKUWA SIZIPOKEI.

Kisha aliongeza,

“SIKUWAHI KUMTAMANI VERA KIMAPENZI WALA SIKUWAHI KUMTAFUTA YEYE NDIO ALINITAFUTA, SINA SABABU YA KUDANGANYA, NILIKAA KIMYA KWA MUDA MREFU SANA …”

Wawili hao walikuwa walikuwa kwenye mahusiano kwa mda wa miezi sita kabla ya kutengana na kilichofuata ni wawili hao kuanikana hadharani kuhusu masaibu yao ya chumbani.

Msanii huyo wa Chaguo la Moyo pia aliwahi sema kuwa Vera aliwahi avia mimba ya mtoto wake.