ILIKUAJE: Usitamani jela kwani kuna magonjwa mengi - King Kafu

kafu na robo
kafu na robo
Leo kwenye kitengo cha Ilikuaje ni bwana Nicholas Cheruiyot almaarufu kama King Kafu, ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Ghetto Radio.

Akizungumza na Massawe Japanni, Kafu alizungumza jinsi alivyojipata katika uhalifu na pia alivyobadilika.

Nimezaliwa Ziwani na kuna siku mwanahabari alikuwa amenyongwa na bidhaa vyake vilikuwa vimeibiwa na polisi wakaja tukakamatwa watu tisa na kupelekwa kwa chifu. Baadaye tukapelekwa kituo cha polisi cha Pangani.

Kafu anasema alikuwa na miaka 11 na sasa alikuwa amesingiziwa kuhusika katika uhalifu na hakuwa na wa kumtetea kwani wazazi wake walikuwa wamefariki.

"Nduguye Juacali ndiye alikuja akanishughulikia na nikatoka jela, lakini wale waliohusika walikamatwa ila hatukuachiliwa lakini mashtaka yakapunguzwa. Ndugu yangu ambaye tulikuwa tumekamatwa naye alianza kuugua na wakti tulitoka tu hivi aliaga dunia."

Kafu anasema alipofungwa miezi mitatu ilimbidi awache shule na kwanza kuuza vyuma. Alipofikisha miaka 17 ndipo alianza wizi wa simu, na bidhaa vingine.

Baadaye walianza kunyonga watu haswa wenye walikuwa wanaenda mashinani au wametoka mashinani kwani walijua wana fedha tele.

Tulifanya kwa kipindi cha miaka mitano ambapo tulikuwa tunakamatwa tunalala gerezani, tunatoka na tunaendelea. Kafu alisema akidai kuwa alibadilisha maisha yake mwaka wa 2006.

Kuna siku tulipata watu wanaenda matanga na tukala fedha zao 250,000 baada ya kuanza wizi wa bunduki. Tulipata wamama wamekwamia begi zao na kumbe walikuwa na stakabadhi za kuenda kuwachilia mwili.

Kafu anasema kuwa anajuta sana maisha hayo haswa akikumbuka kuna siku walivamia gari ambalo lina mama mja mzito na bwanake. Walichukua funguo za ile gari na kutupa ili asipige ripoti.

kilichonibadilisha ni chenye nilijionea kule jela, kisha nikitizama habari naona marafiki zangu wameuawa. Hapo nikaamua nitang'ang'ana niende katika kituo cha polisi niwaambie nimewacha uhalifu na waniskize.

Hapo ndipo alianza kufanya vibarua na pia akaanza kuunda sanduku za wafu kabla ya rafikiye Robert kum