Ilikuaje: Enosh Momanyi alidhani ameteuliwa katika baraza la mawaziri

enosh.momanyi
enosh.momanyi
"Rais alipo kuwa akifanya mabadiliko katika baraza la mawaziri wiki iliyopita nilikuwa nmesafiri nyumbani,

"Ndipo rafiki yangu aliweza kunipigia simu na kuniuliza kwani sijaingia katika mtandao wa kijamii nione vile watu wananipongeza kwa kuteuliwa na rais kufanya kazi," Enosh Alieleza.

Ni makosa ambayo yalitokea wakati rais Uhuru alipokuwa akibadilisha baraza la mawaziri wiki iliyopita.

Rais aliweza kumchagua Enosh Momanyi lakini majina yalikuwa yamefanana na kisha habari zikachapishwa kwa mtu ambaye hakuwa amechaguliwa.

Enosh alisema kuwa alipatwa na mshtuko mkubwa kwa maana hakuwa ametarajia kuwa rais kumjua kwa maana yeye ni kujana wa kawaida.

"Nilishtuka sana nilipoona habari hizo," Alisema Momanyi.

Baada ya habari hizo kutokea Enosh alijandaa na kuweza kumshukuru Rais kwa uteuzi wake.

"Nilijiandaa na kuenda kumshukuru rais lakini baada ya masaa ishirini na nne ripoti zilitokea na kuambia kuwa simimi niliweza kuteuliwa,

"Nilishtuka kwa sana kwa sababu niliweza kufa moyo kwa wakati huo, lakini nampongeza aliyechaguliwa kaika kufanya kazi hiyi,

"Kama ningepata kazi hiyo ningefanya na kushauri vijana wale wengine waweze kujikakamua," Alisema Momanyi.

Wakati huo Enosh aliweza kumpigia mamake na kumfahamisha kuwa si yeye wala ni mtu mwingine.

"Nilipojua si mimi nilijua ata kama si mimi kuna siku itafika nijulikane na nifanyie serikali kazi,

"Nataka kumwambia Rais kuwa katika agenda zake aweze kuweka ajira kwa vijana,

"Hii ni kwa sababu kuna vijana wengi hapa nje ambao hawana kazi na wamesoma," Alizungumza Enosh.

Enosh aliweza kumaliza chuo kikuu mwaka wa 2012,lakini hakuweza kupata ajira bali aliweza kuanzisha kazi ya ujenzi ili kujimudu.

"Nilipojua si mimi sikutaka hata kuangalia simu kwa maana najua kuna watu wengi watasema mambo yasiyofaa,

"Sikuweza kulia lakini nilisema kuwa kama si mimi leo kesho ni mimi," Enosh Aliongea.

Enosh alisisitiza na kusema kuwa serikali inapaswa kuanzisha kazi kwa vijana.

"Sikuweza kupata mbinu za kuzungumza na Rais Uhuru moja kwa moja, ningepata mbinu yeyote haingechukua muda mrefu kukubaliana na maoni yangu kuhusu vijana," Enosh alieleza.