Sonko Alifanyia marekebisho baraza lake la mawaziri- Charles Kerich arejeshwa afisini

Kerich and sonko
Kerich and sonko
 Gavana wa Nairobi Mike Sonko amelifanyia mabadailiko baraza lake la mawaziri .Kupitia arifa  iliyotolewa ijumaa ,Sonko Amemrejesha afisini  Charles Kerich kama waziri wa  ardhi  na mohammed Dgane amerejeshwa katika idara ya barabara . Pauline Kahiga aliyekuwa akihudumu kama waziri wa Ardhi na Fedha amefurushwa .

Larry wambua  ambaye alikuwa akihudumu katika idara ya ugatuzi sasa amehamishwa hadi katika ile ya mazngira .Vesca Kangogo ambaye amekuwa akihudumu kama waziri wa mazngira na kaimu waziri wa afya amehamishwa hadi katika wizara ya ugatuzi .

Hitan Majevda sasa ndiye waziri wa kaunti wa afya ilhali  Newton Munene  na  Lucia Mulwa  wamesalia katika nafasi zao za ICT na elimu mtawalia .Winfren Gathangu  pia ameonyeshwa mlango baada ya kufutwa kazi kama waziri wa kilimo .Sonko  amewateua  George Osewe (Biashara ) na Karen Nyamu  kujiunga na baraza lake la mawaziri . Mwaka jana Sonko aliwasimamisha kazi maafisa 16 wakuu wa kaunti baada ya mkasa wa kuanguka kwa shule ya  Precious Talent Academy na kusababisha vifo vya wanafunzi wanane .