Babu Owino: Hakimu Francis Andayi ajiondoka kutoka kesi ya kujaribu kuua

Hakimu mkuu Francis Andayi amejiondoa kutoka kesi ya jaribio la kuua inayomkabili mbunge wa Embakasi Babu Owino.

Akitaja sababu za kujiondoa kusikiza kesi hiyo, Andayi alisema kwamba mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) alikuwa ameandika barua kwa bodi ya kutathmin kesi katika idara ya mahakama akilalamikia dhamana aliompa mbunge Babu Owino.

Kesi hiyo sasa itachukuliwa na hakimu Bernard Ochoi, baada ya kukabidhiwa kesi hiyo na Andayi.

Hoja hii itatajwa tarehe 2, mwezi Machi mwaka huu.

Babu Owino aliachiliwa na mahakama ya Milimani kwa dhamana ya shilingi milioni 10. Pia aliagizwa kutojihusishwa na kileo chochote katika eneo lolote la umma wakati kesi hiyo ikisikizwa.

Kiwango Fulani cha dhamana hiyo kilikuwa kitumike kugharamia matibabu ya DJ Evolve ambaye alipigwa risasi shingoni na Babu Owino katika B-Club , Januari tarehe 17 mwaka huu.

Alishtakiwa kwa kosa la kujaribu kumuua DJ Evolve na matumizi mabaya ya bunduki.