Sina kinyongo naye,asema Rayvanny

vanny boy
vanny boy

NA NICKSON TOSI

Msanii kutoka lebo ya WCB  Rayvanny amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na bifu yake iliyopo baina yake na Harmonize.

Katika mahojiano na mtandao mmoja Tanzania,Vanny alisema kuwa alikuwa anamlinda Harmonize wakati mtafarujku baina yake na uongozi wa WCB uliokuwa unatibuka na hakuwa na ufahamu kuwa Harmonize alikuwa anawazia mengine.

Kulingana na Vanny boy.,alimshauri mwenzake vya kutosha kabla ya ya kufanya uamuzi wa kutoka kwa lebo hiyo ikiwemo Harmonize kulinganishwa na Diamond.

“Nilikuwa na complain kubwa ingawa siwezi kuionesha kwenye management. So most of the time, Harmonize alikuwa ananipigia simu kucomplain na mimi nilikuwa namwambia bwana hichi kinachotokea si fair lakini kama unaondoka na mungu Kaplan kwamba utafanikiwa, basi utafanikiwa. So if unaenda, ondoka for good usitake iwe na vita,” alisema Rayvanny

Baada ya Harmonize kutoka katika lebo ya WCB,Rayvanny alikuwa na tamasgha ambalo alikuwa ameanda kule alikozaliwa Mbeya bila kulipa ,muda mfupi baadaye Harmonize akatundika picha yake akisema tamasha hiyo yake aliyokuwa anaifanya aliilipia na haukuwa mkutano .

Usemi ambao Harmonize alisema ni kama matusi kwake kwani alihisi kama ametakanwa.

“Mimi nikawa na show yangu nafanya Mbeya. Ni show amabayo nilidecide kufanya kwa ajili ya watu wa Mbeya, nyumbani kwetu. Mimi si kwamba nina hela hizo lakini akaunti yangu mwenyewe iliteteleka mradi nihakikishe kwamba nimekamilisha show ya Mbeya, imenicost sana mpaka imekamilika na nashukuru mungu ilifanikiwa. Jioni nikaja kuona picha kaposti ya video yake alafu kaandika huu sio mkutano wa hadhara, hii ni show watu wamelipa, yaani ile iliniumiza sana,” alisemaVanny Boy._