Ilikuaje:Mke wangu alinimwagia asidi usoni kwa kumzuiya kubeba baadhi ya sehemu za mwili wa mtoto wao aliyekuwa ameaga.

IMG_0822
IMG_0822
Katika kitengo cha ilikuaje Dan alichukuwa fursa yake na kueleza jinsi mkewe alimumwagia asidi[acid] kwenye uso wake hali iliyomfanya kuwa kipofu baada ya kumzuiya kubeba baadhi ya sehemu ya mwili ya mtoto wao aliyekuwa ameaga dunia.
"Mzozo wetu ulianza baada ya kifungua mimba wetu wa kwanza kuaga dunia baada ya kuugua, mke wangu alikuja akaniambia kuwa anataka kupeleka viungo vya mtoto wetu nyumbani, nilikataa na kisha tukasuluhisha maneno

Baada ya hapo nilienda kazini, niliporudi nilienda kulala kilicho nishtua baadae ni uchunguzi wenye ulikuwa usoni mwangu, mke wangu alikuwa amenimwagia asidi." Alieleza Dan.

Akiwa katika mahojiano Dan alisema kuwa alikaa hospitalini kwa muda wa miezi sita na baada ya kutoka aliambiwa na madaktari hawezi ona tena kutokana na madhara yaliyosababishwa na asidi hiyo.

"Nilipotoka hospitali nilipeleka kesi mahakamani, baada ya kukamatwa aliachiliwa kwa dhamana na yuko huru sasa, nilipomuuliza nini kilicho mfanya afanye kitendo hicho aliniambia alidanganywa

Tangu hiyo siku alinipogia simu akiniomba msamaha, na nikamwambia kuwa nimemsamehe kutoka kwa moyo wangu

Hata dada zake walinipigia simu pia na nikwaambia nishaawasamehe, watu wengi sana walishtuka waliposikia kitendo hicho ambacho aliyekuwa mke wangu alikitenda.

Hii ni kwa sababu ndoa yetu ilikuwa ya kupigiwa mfano tulikuwa tunapendana sana." Aliongea Dan.

Wakati huo Dan alipofanyiwa kitendo hicho alikuwa na miaka 26 na mkewe 24  mwaka 2013 /9/21.

"Tulikuwa tumekaa kwa ndoa kwa miaka mitatu nilipofanyiwa kitendo hicho, tangu ni chomwe na asidi ni zaidi ya miaka mitatu 

Kwa sasa sijapata mchumba mwingine lakini nilimsamehe kutoka kwa roho yangu." Alizungumza Dan.