Coronavirus: Mwanamfalme Charles wa Uingereza apata maambukizi ya virusi

Mwanamfalme Charles amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona, umeeleza ufalme.

Mwanamfalme huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 71, anaonyesha dalili ndogo za coronavirus kwa sasa "lakini bado amebakia kuwa katika afya nzuri ", amesema msemaji.

Mkewe The Duchess of Cornwall, mwenye umri umri wa miaka 72 pia amefanyiwa vipimo , lakini vimeonyesha kuwa hana virusi hivyo.

Makao yao ya Ufalme Clarence House yamesema kuwa Charlesna Camilla kwa sasa wamejitenga binafsi katika makazi ya Balmoral, na kuongeza kuwa mwanamfalme "amekua akifanyanyia kazi nyumbani kwa kipindi chote cha siku chache zilizopita ".

Taarifa rasmi imesema: "Kulingana na ushauri wa serikali na wa kimatibabu, mwanamfalme na mkewe the duchess kwa sasa wamejitenga katika makazi katika Scotland.

"Vipimo vilichukuliwa na mamlaka ya kitaifa ya huduma za afya nchini Uingereza (NHS) eneo la Aberdeenshire, ambako walitimiza vigezo vya kupimwa.

"Huenda isiwe rahisi kutambua mwanamfalme aliambukizwa na nani virusi ikizingatiwa idadi kubwa ya watu ambao aliokutana nao katika kazi zake za umma katika wiki za hivi karibuni."

Image caption Mwanamfalme Charles na mkewe Camilla kwa sasa wamejitenga katika nyumba yao

Wafanyakazi kadhaa katika ofisi ya mwanamfalme ya Birkhall na makazi yake ya Balmoral - kwa sasa wamejitenga katika nyumba zao wenyewe.

Msemaji wa mwanamfalme amezungumza na Malkia pamoja na mtoto wake - the Dukes of Cambridge na Sussex - na imefahamika kuwa wameipokea taarifa hiyo vema.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni za wizara ya afya na huduma za jamii, kwa sasa kuna visa zaidi ya 8,000 vilivyothibitishwa vya coronavirus nchini Uingereza ingawa idadi kamili ya visa huendaikawa ni ya juu zaidi . Badhi ya wagonjwa 422 miongoni mwao wamekufa.

Mara ya mwisho mwanamfalme alionekana katika shughuli za umma tarehe 12 Machi lakini amekua akifanyia kazi zake nyumbani kwa wiki chacce zilizopita abako aliendesha mikutano ya kibinafsi na watu waliokutana nae wamefahamishwa kuhusu maambukizi aliyoyapata.