Wanasiasa wa humu nchini wanapokea donge nono na bila shaka binti zao pia wanaishi vizuri, nani hataki kupata mke ambaye ana kipato kizuri?
Kwa walio na ukakamavu basi orodha ndio hii hapa;
1.Ngina Kenyatta
Binti huyu wa rais Uhuru Kenyatta na ama Marget Kenyatta alioekana mbele ya umma kwa mara ya kwanza mwaka wa 2013 wakati babake alipokuwa rais. Wakati ambapo ameonekana katika hafla za umma, tumeona wanaume wakimmezea mate akiwemo Eric Omondi .
- Andrea Kenneth
Binti yake Peter Kenneth alisababisha mtikisiko wa mtandaoni alipotambulishwa kwa umma pamoja na kakake Andrew Kenneth wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuwania urais ya babake mwaka wa 2013. Andrew pia aliwavutia wengi kwa kutoa himizo kwa wapiga kura kumchagua babake kuwa rais .
- Lupita Nyong’o
Mshindi huyo wa tuzo ya Oscar ni binti yake gavana wa Kisumu Anyang’a nyong’o. Lupita ni muigizaji wa filamu na ameipa Kenya sifa hasa baada ya hotuba yake iliyopewa wakenya kwamba kila mtu anaweza kutimiza ndoto yake maishani. Anazungumza kihispania, Kiingereza, Luo na Kiswahili .
- Tallisa Moi
Ni mjukuu wa rais wa pili wa taifa Daniel Arap Moi na binti yake Philip Moi. Ametambulika sana kwa kupenda kutumia mitandao ya kijamii na wakati mmoja ulizagaa uvumi kwamba yupo katika uhusiano na mwanawe rais Uhuru Kenyatta .
- Makenna Maria Ngugi
Ni binti yake mwakilishi wa kina mama wa Nairobi Esther Passaris. Makena pia ni msani na mara ya kwanza alitambulika akiwa na umri wa miaka 16 alipoonyesha ustadi wake wa kufoka mistari. Kazi ndio hiyo sasa.