I'm Negative,' Meneja wa Diamond afichua hana corona

Ni habari  njema kwa mashabiki wa meneja wa staa wa Bongo Diamond, Sallam SK Mendez baada ya jamaa huyo kutangaza kuwa amepata nafuu baada ya kuwa chini ya uangalizi kutokana na virusi vya Corona.

Sallam ambaye alionekana mchangamfu alipokuwa anatoa taarifa hiyo kwa wafuasi wake, alifichua kuwa amekuwa chini ya karantini kwa wiki mbili na sasa amepata nafuu.

AFTER 14 DAYS GOT TESTED TWICE AND BOTH RESULTS CAME BACK NEGATIVE AND NOW AM OUT OF ISOLATION CENTRE. THANKS TO ALLAH, THANKS TO DOCTORS, NURSES AND THE GOVERNMENT. Sallam Aliandika.

Sallam ndio mwathiriwa wa  pili wa  Tanzania kupona corona, katika posti zingine alimshukuru Mungu kwa kwa kupata nafuu.

“NIMSHUKURU ALLAH 🙏🏽 NA PIA NIWASHUKURU WOTE MLIONITUMIA MSG, COMMENTS, DM NA DUA ZENU. BILA KUWASAHAU TEMEKE ISOLATION CENTRE KWA KUWA BEGA NA BEGA PAMOJA NA MIE BILA KUNICHOKA PALE NILIPOKUWA NIMEZIDIWA, NA SHUKURANI ZANGU ZINGINE ZIENDE KWA MADAKTARI BINGWA KUJUA MAENDELEO YANGU MARA KWA MARA NA PIA SERIKALI YANGU NA VIONGOZI WAKE HUSIKA WIZARA NA MKOA WALIKUWA HAWANA UBAGUZI KUTUJULIA HALI NA KUTUPA MOYO NA KUTUPA MAHITAJI TUTAKAYO.” Aliandika.

Aliwapa wananchi na hata mashabiki wa ushauri .

“NAOMBA NIWAPE TAARIFA NDUGU YENU, KIJANA WENU NIMECHUKULIWA VIPIMO MARA MBILI NA NIMEKUTWA NEGATIVE NA KWA SASA NIPO HURU. ILA NAOMBA TUENDELEE KUJIKINGA NA KUFATA USHAURI WA VIONGOZI WETU NA KUACHA MAELEKEZO YA UTASHI YASIYOKUWA NA UHAKIKA. ALLAH IS GREAT 🙏🏽🙏🏽🙏🏽”