‘Patient One’: Tazama picha za mgonjwa wa kwanza Coronavirus Kenya ambaye sasa amepona

Mwanadada wa Kenya Ivy Brenda Cherotich ndiye aliyekuwa mgonjwa wa kwanza wa virusi vya Corona nchini.

Leo Brenda, na mgonjwa mwingine Brian wamezungumza na rais Uhuru kenyatta kupitia njia ya Video na kuwapa wakenya matumaini kwamba wagonjwa wa coronavirus wanaweza kupona.

Hizi hapa baadhi ya picha za Brenda kabla hajapatikana katika lindi hili la coronavirus .

‘Madaktari walichukulia kisa changu kwa uzito uliosatahili  na wakanipa  barakoa. Nimekuwa katika karantini kwa siku 23 ,na nilitunzwa vyema’.

Brenda  amewahimiza  wakenya  kuwajibika na  kuripoti kwa mamlaka pindi wanapopata daalili za virusi vya Corona .

Anasema wauguzi wakati mwingine walikuwa chini ya shinikizo na walikuwa wakimuita ‘mgonjwa wa kwanza’.

‘Nilipowasili Kenya  nilikuwa na kikohozi kwa siku tatu, niliendelea kutathmini hali yangu na baadaye nikaamua kwenda hospitali ya Mbaghathi siku ifuatayo’ amesema Brenda.

Brenda aliwahimiza wakenya  kuwajibika na  kuripoti kwa maamlaka pindi wanapopata dalili za virusi vya Corona.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO