Kwa mujibu wa duru za kuaminika katika wizara ya afya ,maspika wa mabunge yote walishauriwa kufutilia mbali vikao vya mabunge yote kwa sababu yay a wabunge walipatikana na virusi hivyo . Baadhi yao walipimwa wiki jana na matoeo ya vipimo hivyo yalitolewa sik ya jumatatu na kuzua hofu katika mabunge yote .
“ Wanashuku wabunge 17 wana virusi hivyo na ndio kwa sababu vikao vya mabunge yote vilisistishwa .tunangoja maelezo kamili’ amesema mbunge maybe hakutaka kutajwa . Majina yao kwa sasa hayawezi kutajwa kwa sababu ni hatia kufichua hali ya kiafya ya mtu bila idhini yake .
Seneta mmoja amesema spika alitangaza kusitishwa kwa vikao vya bunge ili kuzuia kuambukizwa kwa wabunge na masenata zaidi endapo walioambukizwa virusi hivyo wangeruhusiwa kutangamana na wenzao katika bunge .
Maseneta ,wabunge na wafanyikazi wa bunge wamekuwa wakipimwa kwa hiari kujua iwapo wana ugo0njwa huo katika majengo ya bunge tangu wiki jana . Zaidi ya wabunge 200 na maseneta wakiwemo maspika wa mabunge yote wamepimwa virusi hivyo na wameanza kupokea matokeo yao kila mmoja .
Hata hivyo spika wa senate Ken Lusaka amekanusha uvumi huo akisema ni vigumu kujua NI nani ana virusi hivyo kwani kila mtu alipokea matokeo yake kivyake .
Baadhi ya wabunge ambao wamejiweka katika karantini wenyewe ni mbunge wa Eldas Adan Keynan, Naomi Shaban (Taita Taveta), Aaron Cheruiyot (Kericho) na George Khaniri (Vihiga). Walikuwa wamesafiri kwenda Uingereza mapema mwezi uliopita .