Ruth Matete awaambia wapelelezi wa DCI mazungumzo ya mwisho na mumewe

Msanii Ruth Matete alimpoteza mpenzi wa roho yake mchungaji John Apewajoye wiki iliyopita huku maswali yakiibuka kuhusu hali iliyopelekea kifo chake.

Hii ni kwa sababu Ruth alisema kuwa mumewe alimshauri asiweze kusema chochote kwa familia kuhusu kulazwa kwake hospitalini

Mumewe Matete aliaga dunia  kwa ajili ya mejeraha aliyopata  kwa ajili ya   mlipuko wa gesi nyumbani kwao

Ruth alihojiwa na wapelelezi wa DCI na aliwaeleza kuhusu  mazungumzo ya mwisho na mumewe kuhusiana  na  jinsi alivyomzuia asiseme lolote kuhusu kulazwa kwake hospitalini .

Kulingana na wakili wa Ruth Matete, mumewe alimsihi asiwaambie jamaa zake kuwa yupo hospitalini na asijaribu kuwaambia kuhusu  ajali ya mlipuko wa gesi nyumbani kwao

“HE REQUESTED HER NOT TO TELL HIS FAMILY WHAT HAPPENED BECAUSE HE DID NOT WANT THEM TO GET WORRIED. IN HIS FIRST WEEK IN HOSPITAL, HE VIDEO CALLED HIS BROTHER TO ASSURE THE FAMILY THAT HE WAS ON THE ROAD TO RECOVERY. THAT WAS BEFORE HIS WOUNDS BECAME SEPTIC AND HIS KIDNEYS STARTED FAILING." Alizungumza wakili.

Wakili wake alisema kuwa Ruth aliwaarifu jamaa za John kuwa yupo hospitalini kwa ajili ya kidonda cha tumbo kwa lugha ya kimombo 'appendicitis'.

“THEY WERE APTLY INFORMED WHEN HE DIED."

Mara ya kwanza familia yake ilikuwa na shida kwa kutoambiwa ukweli lakini walipoelezewa na wakili wa Ruth kilichojiri walielewa.

Afisa wa DCI kutoka Athi river Vincent Korir alizungumza na kusema hamna mashtaka yoyote  yatakayopendekezwa dhidi ya Matete  na wanangoja ripoti ya upasuaji   wa mwili wa mwendazake .