Wazee hao wamezungumza huku washirika wa Ruto wakianza kupeleka makabiliano dhidi ya rais Kenyatta katika ngome yake na kubadilisha mageuzi katika takriban kaunti mbili yaliodhinishwa na rais . Malumbano ambayo yamekuwa yakitokota katika chama cha Jubilee huenda yakalipuka wakati wowote huku pakiibuka ripoti kwamba rais Uhuru Kenyatta anapanga kufanya mageuzi ya kunadhifisha serikali yake kwa kuwaondoa baadhi ya washirika wa Ruto katika nafasi za uongozi chamani na bungeni .
Wakizungumza na gazeti la kiongozi wa baraza la wazee wa kikuyu Rift valley Gilbert Kabage a na mwenyekiti wa baraza la wazee wa kalenjin Myoot askofu mstaafu Paul Leleito wamedai kwamba Uhuru anamfadhaisha Ruto kupitia washirika wake . Wamedai kwamba kimya cha rais Kenyatta huku naibu wake akipigwa vita ni dhihirisho tosha kwamba ameidhinisha mashambulizi hayo .Kabage amemtaka rais Uhuru kujitokeza wazi na na kutangaza iwapo atatekeleza makubaliano yao ya mwaka wa 2013 kwamba tamuunga mkono naibu wake kuchukua usukani mwaka wa 2022 badala ya kumhujumu .
“ Kile ambacho Uhuru anamfanyia Ruto ni vitendo vya kale ambavyo havina ustaarabu . tumeshuhudiwa machafuko ya kikabila 1992,1997 na mwaka wa 2007-2008 . Tunataka kuwamabia wahusika kwamba hatutakubali kurejeshwa katyika mondo huo tena’ amesema
Wakosoaji wa Naibu wa rais wamekuwa akidai kwamba washirika wake wanatumia vitisho vya ghasia Rift valley ili kuwalazimisha watu wa jamii ya kikuyu kumpigia kura mwaka wa 2022.
“ Iwapo Uhuru anataka kufanya muungano na Raila basi afanye hivyo bila kumfadhaisha Ruto na sarakasi hizi zote . wakenya wataamua kiongozi wao wakati utakapofik’ Kabage amesema
Amesema iwapo Ruto hangemfanyia kampeini rais Kenyatta kwa nguvu zake zote basi Uhuru hangekuwa rais .
“Uhuru anafaa kukumbuka vizuri ‘handshake’ aliofanya na Ruto katika uwanja wa Afraha ,nakuru na ahadi aliotoa . aAlitoa ahadi hiyo mbele ya ummati wa watu na tutaendelea kutii ahadi hiyo’ amesema
Lakini akimjibu mwenyekiti wa baraza la jamii ya wazee wa jamii ya kikuyu Wachira Kiago amesema kauli hiyo ya Kabage ni hatari na isiyo na uajibikaji.
“Uhuru kila mara anazungumzia kuhusu kuwaunganisha wakenya . sasa inakuwa vipi kuna wanaosema kwamba hilo ni kuzigonganisha jamii mbili?’ alihoji
“ Ni jambo la kusikitisha kwamba matamshi kama hayo yametoka kwa wazee . kuna masuala mengine ambayo taifa linakabiliana nayo kwa sasa na wazee wanafaa kuyangazi’ aliongeza .
Naibu wa rais mwenyewe amedai kwamba huenda asasi za utawala na serikali zimegeuzwa kuwa silaha ili kumpiga vita . Amekuwa akikosa kuonekana katika makabiliano ya serikali dhidi ya janga na virusi vya Corona ambavyo vimeathiri uchumi wa taifa. Hivi karibuni hata hivyo Ruto amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kunukuu aya za biblia ili kutuma jumbe fiche kueleza makabiliano dhidi yake na kutoa taswira ya kilicho fikrani mwake .