Wakaazi wa Kangutu huko Isiolo wametamaushwa na kisa cha mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 28 kumkata kichwa mkewe kutumia panga baada ya ugomvi wa kinyumbani .
Baada ya tukio hilo David Kiringori alijisalimisha katika kituo kidogo cha polisi cha Kulamawe akiwa amembeba mtoto wao wa umri wa miaka miwili. Majirani wamesema jamaa huyo amekuwa akimshambulia mkewe kila mara na wakati mwingi marehemu alikuwa akitoroka kuokoa maisha yake .
Kamanda wa polisi wa kunti ndogo ya Isiolo George Kariuki amesema mshukiwa alizuiliwa katika seli mara moja na mwili wa mkewe umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Isiolo. Mkuu huyo wa polisi amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo ili kutambua kilichosbabisha mauaji hayo .