Dereva wa lori atoweka baada ya kupatikana na corona

power.blackout-508x300
power.blackout-508x300
Serikali  ya Uganda imeanza kumtafuta dereva wa lori kutoka Kenya aliyekuwa amethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona na kutoweka. Dereva huyo aliingia nchini humo tarehe 8, Mei na kupimwa virusi hivyo katika eneo la Malaba.

Dereva huyo aliacha gari lake na kutoweka baada ya kugundua ana virusi vya corona.

Msemaji wa polisi wa Uganda Patick Okemo siku ya Jumapili aliwataka wananchi kujitolea na kutoa habari kumhusu dereva ili atiwe nguvuni.

"Juhudi za kumsaka mgonjwa ambaye ameenda mafichoni zinaendelea. Kikosi cha usalama na maafisa wa afya wanamsaka jamaa huyo.  Vita hivi si vya maafisa wa usalama na wa afya pekee," Okemo alisema.

Mnamo tarehe 10, Mei, nchi ya Uganda ilikuwa imethibitisha visa 121 vya corona ambapo watu 55 walikuwa wamepona kutokana na virusi hivyo.

Uganda ilianza mchakato wa  kuwapima madereva wa masafa marefu baada ya madereva wanne kutoka nchi jirani ya Tanzania kupatikana na virusi hivyo nchini Uganda.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO