'Wanawake wa mbali siwawezi.' Juma Jux aeleza sababu za kutengana na mpenzi wake

Mapema mwaka huu, uvumi ulienea sana kwenye mitandao ya kijamii kuwa msanii wa nchi ya Tanzania Juma Jux alitengana na mpenzi wake Nayika Thongom, lakini huo ulikuwa tu uvumi.

Wengi waliulizana nini kilichosababisha  kutengana kwao na watakuwa vipi kama hawako  pamoja. Kwa sasa, Juma hayupo tena na mpenzi wake.

Akiwa katika mahojiano, Juma alieleza sababu zake za kutengana na mwanamke huyo, lakini sababu ni ipi haswa iliyosababisha wawili hao kuachana?

Haya basi hii hapa sababu yake;

"It didn’t work out. Long-distance is so difficult; I can’t. Now, sitaki wanawake wa mbali. Wanawake wa mbali siwawezi anymore.Nayika was from Thailand. I had known her for a while then we got serious. The thing is, distance; she can’t move here, I can’t move there. We got to a point it became too much. I personally dislike video calls, chatting every time- so it became difficult." Alieleza Juma Jux.

Jux aliyefahamika sana na mashabiki wake kwa wimbo wake wa 'Utaniua',  hakukimya bali alifichua na kueleza kile anachotaka kutoka kwa mpenzi wake ambaye atakuwa naye.

“I don’t choose as to where she comes from. First,naangalia kichwani before anything else. Uzuriwake uanzie kichwani; awe smart sana. She has to very smart, to challenge me sometimes and independent. When I say independent it is not that I am avoiding to take care of her but I believe that a woman who has her own life finds it easy to be confident with herself. I can provide for her as her boyfriend or man but she has to hustle too." Alizungumza.

Juma alianza kumchumbia Nayika baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee ambaye sasa ni mpenzi wa Rotimi.

Imehaririwa na Yusuf Juma