Watu 23 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kupimwa na serikali

OWHtHGLk
OWHtHGLk
Chini ya saa 24, serikali imefanyia watu 2, 100 vipimo na kati ya hao watu, 23 wamepatikana na virusi hivyo na kufiksha idadi ya wale walioambukizwa nchini kuwa watu 781.

Wakati uo huo, katibu msimamizi katika wizara ya afya Dr Rashid Aman amesema watu wengine watatu wamefariki na kufikisha watu waliokufa nchini kutokana na virusi hivyo kuwa 45.

Visa hivyo vipya vimetokea katika maeneo yafuatayo pamoja na mitaa husika Nairobi - 11 (Embakasi-6, Kamukunji-2, Lang'ata-2, Starehe-1), Mombasa - 5 vyote vikitokea Mvita, Kajiado - 3 wakiwa na madereva wa magari kutoka Namanga  Kiambu - 2 (Thika) Wajir - 2 kutoka Wajir Mashariki.

Aman amesema kuwa masharti yaliyokuwa yamewekwa na serikali yanafikia kikomo na serikali itatoa taarifa zaidi hiyo kesho.

Aman ameongeza kuwa serikali inaendelea na kupima madereva katika mipaka yake ili kukabiliana na janga hilo.

Amesifia wakenya ambao wametilia maanani masharti yaliyowekwa na serikali akisema itasaidia pakubwa kupunguza maambukizi hayo.

Amesema mipango ya kuwapima wananchi itaanza na kuwarai wale ambao wanaishi karibu na mipaka nchini kuwa macho dhidi ya wale wanaoingia nchini kutoka mataifa jirani