Serikali ilizifunga shule zote mwezi machi kwa sababu ya janga la coronavirus na tathminmi ya wizara ya afya kwamba huenda virusi hivyo vikafika kilele chake mwezi agosti inamaanisha kwamba muhula wote utakuw umekwisha bila wanafunzi kurejea shuleni .
“ Mitihani ya kitaifa inafaa kuahirishwa hadi wakati watahiniwa watakapokuwa tayari kuifanya .wiki kadhaa za masomo imepotea kwa sababu shule zilifungwa ghafla ,itakuwa muhimu baada ya shule kufunguliwa mikakati ifaayo iwekwe ili kuwapa wanafunzi maagizo ya kuweza kujifunza yote waliokosa’ muungano wa walimu wakuu umesema
Kalenda ya baraza la mtihani nchini KNEC inaonyesha kwamba mtihani wa KCPE utaanza oktoba tarehe 27 ilhali ule wa KCSE utaanza Novemba tarehe 2.
Rais Uhuru Kenyatta na waziri wa Elimu George Magoha wamesema kwamba kalenda ya mtihani kwa watahiniwa wote milioni 1.8 itasalia jinsi ilivyopangwa .