Wapende wasipende kura ya Maoni ni huu mwaka- Raila Odinga

Kinara wa chama  cha ODM Raila Odinga amesema ni lazima kufanyike kura ya maoni mwaka huu yaani Refendum kabla ya mwaka huu haujatamatika.

Matamshi yake yanajiri saa chache tu baada ya seneta wa Siaya James Orengo na ambaye pia ni kiranja wa wachache katika bunge la seneti kusema kuwa ni sharti mabunge yote mawili kujadili pendekezo hilo chini ya miezi ijayo.

Shughuli za kuhamasisha umma kuhusiana na ripoti ya pamoja ya BBI ilisitishwa kwa muda kutokana na virusi vya corona ambapo serikali ilipiga marufugu shughuli za watu kutangamana kwa mikutano nchini.

 Raila  alisema kura hiyo ya maoni itafanyika mwaka huu japo akasisitiza kuwa ni sharti taifa liwe limeimarika katika sekta ya uchumi ambayo imedorora kwa asilimia kubwa.

“I see a referendum happening before the end of this year…it is possible before the end of the year,” amesema Raila akiwa kwa mahojiano na kituo cha redio moja ya humu nchini.

Miongoni mwa mapendekezo ya jopokazi kuu lililoteuliwa la BBI ni kupanuliwa kwa nyadhifa za uongozi ili kubuni nafasi ya waziri mkuu..

Aidha Raila amesema kuwa lengo kuu la BBI ni kuliunganisha taifa na kuimarisha maisha ya mkenya wa kawaida.

“These situations have brought poverty, diseases and joblessness, hence our call to the government to take steps to restore the economy,”amesema Raila.

Amepusilia mbali baadhi ya viongozi ambao wameanza kuweka mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 akisema ni sharti watu waangazie BBI kwanza.

Raila amempongeza kiongizi wa taifa Uhuru Kenyatta kwa kufufua uchumi wa taifa baada ya kutenga kapu la bilioni 54 ili kufanikisha utendakazi wa sekta mbalimbali nchini.

“These must be dealt with first before we return to reggae. We can’t return to politics when people are still hungry,” Raila

Ameongezea kuwa ni vyema viongozi waache kuendeleza ajenda za siasa kwa wananchi ambao wanakumbwa na njaa.

“And as they say, a hungry man is an angry man. We wouldn’t want to take politics to angry people,” Raila alisema

Ameongezea kuwa uhamasishaji wa watu kuhusiana na BBI haujasistishwa kamwe.

“We said no one can stop reggae. It has not been stopped. Covid-19 is not a person. Reggae is on half-time. It will come back soon,” Raila

Kabla ya kusitishwa kwa BBI, kaunti kutoka Nyanza ,Magharibi, Pwani ya Kenya, Kaskazini, Kutoka Jamii ya Maa, Garissa na Meru zilikuwa zimeanda hafla ya mikutano ya BBI.

Kaunti ya Nairobi na   Rift Valley ndizo zilizokuwa zimesalia kuwasilisha mapendekezo yao.