Hotuba ya Rigathi Gachagua yatibuliwa na polisi kwa mazishi Nyeri

NYERI-BURIAL-POLICE
NYERI-BURIAL-POLICE

Mbunge wa Mathira Rigath Gachagua amelazimika kukatiza hotuba yake katika hafla ya mazishi yaliyokuwa yanafanyika katika kaunti ya Nyeri baada ya waombolezaji kukosa kutii amri ya serikali ya kuruhusu watu 15 wa familia kuhudhuria mazishi hayo.

Gachagua alilazimika kukatiza hotuba hiyo wakati wa maishi ya mke wa mwakilishi wa wadi Erick Wamumbi ,Catherine Nyambura baada ya polisi kuingia ghafla na kusitisha mchakato huo mzima.

Amepinga  hatua hiyo ya polisi akisema kuna baadhi ya viongozi ambao waliruhusiwa kuanda kongamano hiyo jana na hivyo ni sharti wangeachilia familia na watu wa karibu kumpatia mkono wa buriani mwendazake.

“The government should employ uniformity in dealing with social gatherings,” “Yesterday, we saw Atwoli and others hosting huge crowds why are they denying us yet we are Kenyans like them,” amesema  Gachagua.

Mumwe mwendazake alilazimika kuwaomba maafisa hao wa polisi kumwachilia Gachagua baada ya kushuhudiwa  mvutano baina yao

Gachagua ambaye ni mmoja wa wabunge wanaogemea upande wa naibu rais alisema ni sharti watu waruhusu wengine kuwa na misimamo tofauti ya kisiasa..

“People should be allowed to make their own political decision and already others have done so. Why all this drama,” alisema.

Wabunge Moses Kuria ,  Kimani Ichungwa na  Ndidi Nyoro,walikuwa wanatarajia kuhudhuria mkutano huo japo wakakosa.