Polisi wamuuwa mwanamgambo wa Al Shabaab Diani- Kwale

Maafisa wa polisi walimuwa jamaa mmoja anayeshukiwa kuma mmoja wa kundi la kikaidi la Al- Shabaab  katika eneo la Diani kaunti ya Kwale .

Miongoni pia mwa wale ambao wameuwawa ni watoto wa jamaa huyo wawili ambao alikuwa anawatumia kujikinga dhidi ya marisasi yaliyokuwa yalitokea upande wa polisi hao.

Mohamed Mapenzi alitambarizwa katika nyumba yake na polisi hao taarifa ambazo zimeripotiwa na Daily Nation.

Kulingana na taarifa hiyo ,jamaa huyo alikataa katakata kujisalimisha na hata kuamua kuwarusha maafisa hao vilipuzi ,huku afisa mmoja akijeruhiwa .

Hapo ndipo maafisa hao waliamua kumfyatulia marisasi na kumuuuwa pamoja na wanawe wawili .

Mkewe na wanawe wengine watatu wanaendelea kupata tiba baada ya kupata majeraha madogo madogo katika patashika hiyo.