Ni mdau wa muziki wa bongo,'Hisia za Alikiba baada ya Rayvanny kusema anapenda kibao chake cha 'dodo'

FWJk9kpTURBXy8yYjVjZDdkZWYyZTU0ZjNmMmRjNGM5YjliMzZmMmQ3OS5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB
FWJk9kpTURBXy8yYjVjZDdkZWYyZTU0ZjNmMmRjNGM5YjliMzZmMmQ3OS5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Msanii wa bongo Alikiba amezungumza na kumjibu msanii mwenzake Raymond Shaban almaarufu Rayvanny baada ya kusema kuwa anapenda sana kibao chake cha 'dodo' ni kibao alichokitoa hivi majuzi na kuwavutia wengi.

Akizungumza kwenye mahojiano na Bongo5 alisema kuwa matamsho ya Vanny boy yanaonyesha kuwa ni shabiki wa muziki wa Bongo flavour.

Ali Kiba alimshukuru Rayvanny na kusema pia naye husikiza baadhi ya nyimbo za Rayvanny na kuimba wimbo wake wa 'kwetu na 'natafuta kiki' alizosema kuwa ni nyimbo ambazo anapenda sana za Vanny Boy.

“Huyu alikiba Dodo right. Kwenye kumi ntampa kumi. Btw this is my favorite song kwa Alikiba, napenda Dodo." Rayvanny Alisema.

Kibao cha 'Dodo cha Alikiba kimesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii huku mashabiki wengi wakikipenda na kusema kuwa Alikiba aliweza na kibao hicho.