Uchunguzi wa kifo cha Tecra Muigai kuchukua siku 30 zaidi

afed5cefd9f173e8
afed5cefd9f173e8
Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai, DCI imewapatia maafisa wanaochunguza mauaji ya mrithi wa kampuni ya Keroche Tecra Muigai siku 30 kukamilisha uchunguzi dhidi ya mshukiwa mkuu Omar Lali.

Lali mwenye umri wa miaka 54 alikuwa mpenzi wa marehemu na walikuwa wakiisha pamoja mjini Lamu kabla ya kifo chake.

Tecra alipata  majeraha mabaya kwenye kichwa chake baada ya kuanguka kutoka kwa ngazi ya nyumba aliyokuwa akiishi.

Kikao cha mahakama kilichofanyika Jumatano, Juni 10 kupitia njia ya video kikiongozwa na hakimu wa Lamu Allan Temba na wakili wa Lali Yusuf Aboubakar kiliafikiana na mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, DPP na wa Upelelezi, DCI kuchunguza kesi hiyo kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Hata hivyo, Lali ataendelea kuwa huru huku uchunguzi dhidi yake ukiendeshwa. Chini ya saa 24 baada ya kifo cha Tecra, Lali alikamatwa na kuzuiliwa kwa siku 21, aliachiliwa huru baadaye kwa dhamana ya KSh300,000 mnamo Mei 27.

Lali amekana mashtaka dhidi yake na aliambia mahakama kuwa hangemuua mtu ambaye alikuwa kipenzi cha roho yake.