Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na gavana wa zamani wa Bomet Isaac Rutto walikuwa katika hafla hiyo katika makao makuu ya chama cha Jubilee . Katibu mkuu wa chama cha Judith Sijeny amesema lengo lao kujiunga na Jubilee kupitia makubaliano hayo ya ushirikiano ni kuwaleta watu pamoja . Mwezi uliopita baraza kuu la usimamizi wa chama cha Wiper Lilimpa kalonzo Idhini ya kusainia makubaliano ya kushirikiana na Jubilee . Mwafaka uliafikiwa baada ya mkutano uliofanywa kupitia njia ya video na zaidi ya watu 50
Wanachama hao waliunga mkono kwa kauli moja kutekelezwa kwa mkataba huo wa ushirikiano huo. Wakati wa mkutano huo Kalonzo amesema makubaliano hayo haumaanishi kwamba wamejiondoa kutoka muungano wa NASA .
Mkataba huo unajiri baada ya chama cha Kanu pia kusaini mkataba wa ushirikiano nan a Jubilee. Mkataba huo wa Kanu na Jubilee ulifanikisha kuteuliwa kwa seneta wa West Pokot Samuel Poghisio wa Kanu kutajwa kuwa kiongozi wa walio wengi katika senate .
Mwezi ulipita Rutto alifichua kwamba alikuwa akijadili mkataba wa ushirikiano wa kisiasa na rais Uhuru Kenyatta .Rutto ni mshirika wa karibu wa seneta wa Baringo Gideon Moi ambaye pia chama chake cha KANU kipo katika makubaliano ya kisiasa na Jubilee .