Back with A bang!Marya Prude ajitokeza baada ya kutengana na Willis Raburu

Mamepa mwezi mei  palizuka habariu za kutengana kwa Marya Prude na mumewe Willis Raburu na hata kipusa huyo akalazimika kuondoka nyumba waliokuwa wakiishi pamoja katika barabara ya Kiambu .

Habari za kutengana kwao zilisambaa mitandaoni kama moto katika kichaka kikavu  na  kwa sababu Marya ni mtu anayependa usiri wake alilazimika kujiondoa kwa muda kutoka mitandao ya kijamii . . Lakini kutokana na hatua alizochukua wiki hii yaonekana ameanza kureja tena mitadaoni na hata labda kupona makovu yaliyotokana na kutengana kwao .

Hakuna kati yao aliyezungumza kuhusu kilichotokea  lakini labda kuna jambo zuri kuwa na matumaini katika masuala ya mapenzi .

Willis Raburu  na  Marya Prude  walifunga ndoa miaka mitatu iliyopita  na wameyapitia mengi tangia hapo ikiwemo kumpoteza mtoto wao  aliyekuwa amezaliwa .