Madaktari hawajathibitisha kama mcheshi Othuol Othuol ana uvimbe au la

Mwenyekiti wa Jamii ya ucheshi humu nchini Ken Waudo amezungumzia afya ya mcheshi Othuol Othuol ambaye amekuwa amelazwa hospitali kwa muda sasa.

Othuol alilazwa hospitali mnamo tarehe 24 Juni baada ya kuzirai akiwa nyumbani kwake.

Waudo akizungumzia hali yake alisema kuwa madaktari hawajabaini wala kuthibitisha kuwa Mcheshi huyo ana uvimbe wa ubongo au la,

“The first MRI scan for the hospitalized Comedian Ben Maurice Onyango popularly known as Othuol Othuol results were released and indicate he has an abnormal infection in the brain. The medics told us they could not confirm if it's a tumor or not.Consequently this means he will remain under hospital scrutiny for the next 6 WEEKS as well as under medication as subscribed. Within a period of two weeks from now, he'll have to undergo another MRI scan if there's no change." Alizungumza.

Mcheshi Othuol amekuwa akilazwa hospitali kila mara na kutoka baada ya kupata nafuu, Waudo alisema kuwa kama jamii ya ucheshi watahakikisha kuwa Othuol amekuwa sawa.