Mwanamke mmoja yuko chini ya shinikizo kurudisha pesa za Harambee baada ya bwana harusi kuhepa nazo

AUMA
AUMA
Agosti mwaka 2018, Irene Auma, mkaazi wa  Likoni, Mombasa,alitarajiwa kufunga pingu za maisha namumewe ambaye alijulikana kama John Nelson Juma.

Harakati za kupanga harusi hiyo zilikuwa zimeshika moto hadi wiki tatu kufanyika kwa harusi hiyo ambapo Auma wa miaka 24 alifahamu kuwa mumewe  Juma alikuwa ameamua kubadili uamuzi wake na kuamua kumuoa bindti mwengine.

Kulingana na Auma na taratibu za kiafrika,Auma na mpenziwe walitoa mgao fulani wa fedha huku marafiki na jamaa zao wa familia wakitoa shilingi 30,000 ambazo zilipewa Juma mpenziwe wakati uo.

Wiki tatu kufanyika kwa harusi hiyo,Auma anasema kuwa Juma alimfahamisha kuwa amebadili nia ya kumuoa na kutokana na ushauri aliokuwa amepewa na marafiki wake alishauriwa kuoa mwanamke mwengine.

Baada ya mipango ya harusi kutibuka ,Auma amesema amekuwa akimtafuta Juma kwa muda ili arudishe pesa hizo bila mafanikio yoyote.

“I am under a lot of pressure to refund the monies,” she said, adding: “every other time I meet the people who contributed to our aborted wedding, they usually remind me to give them back their money”.

Anasema anafahamu kuwa mpenziwe huyo alifunga pingu za maisha kitambo na hivyo ni vyema arudishie familia na marafiki waliokuwa wamechangia pesa zao.