Wakenya wanafaa kujitayarisha kwa kura ya maoni licha ya kuwepo janga la corona viongozi kadhaa kutoka magharibi wamesema .wakiongozwa na aliyekuwa maneja wa kampeini za gavana Wilber Otichilo Joseph Simkha ,viongozi hao wamesema wakenya wanafaa kuzoea maisha licha ya kuwepo kwa virusi hivyo na nidhamu ya hali ya juu itahitajika ili kuzuia maambukizi zaidi .
Wanatataaluma hao walikuwa wakizungumza Ebunangwe Resort katika eneo bunge la siku ya ijumaa .
" Mataifa mengine yameandaa uchaguzi wakati huu wa corona .Ufaransa na Malawi zimefanya hivyo vizuri na Tanzania pia huenda inaelekea kuchukua hatua kama hiyo’ amesema Simekha .
“ iwapo wakenya watapewa fursa ya kupiga kura ,wasipuuze maagizo ya serikali kuhusu coronavirus ,tumeona athari za virusi hivyo kote duniani’ alisema
Kuhusu mchakao wa BBI Simekha amesema sio tu kuhusu uongozi bali pia ni njia yay a kuboresha uchumi wa taifa .
Wanataaluma hao wamesema kuna haja ya kuwahusisha katika mchakato huo mzima ili kuzuia wanasiasa kuwapotosha waenya . wameongeza kwamba BBI inalenga kuimarisha ugatuzi .