'Namuombea Mola ampe mwanamke wa kuoa aache kurukaruka,'Diamond ashauriwa na baba yake huku akimsifu Alikiba

diamond-na-babake
diamond-na-babake
Mzee Abdul Juma ambaye ni baba yake staa wa bongo Diamond Platnumz amemshauri mwanawe aache kurukaruka na kuwachezea wanawake bali anapaswa kutulia na mwanamke mmoja.

Huku akiwa kwenye mahojiano na SNS alimshauri mwanawe afuate mienendo ya msanii mwenzake Alikiba.

"Anapaswa kutulia na awache kurukaruka hapa na pale, namuombea Mola ampe mwanamke ambaye anaweza kuoa ana uwezo wa kuoa sasa kwa maana ni mti mzima sasa." Alizungumza Juma.

Aidha Mzee Juma aliendelea na kumsifu msanii Alikiba,

"Kama vile Alikiba ameoa tayari na ametulia Diamond anapaswa kutulia chini na kuacha mambo ya kidunia yaendelee kwa hakika sijui shida yake iko wapi naomba tu Mola amuwezeshe atulie."

Hata hivyo Mzee Juma ana furaha tele baada ya Diamond na Zari kutupilia ugomvi wao mbali na kuanza kusaidiana kulea watoto wao.

Haja yake kubwa ni kuwaona wajukuu wake Princess Tiffah na Prince Nillan,

"Sipendi kabisa watu wanapobishana, mahusiano yana mambo mengi sana na jambo moja mmoja anapaswa kuwa  mnyenyekevu, nina furaha sana kwa maana wametupilia ugomvi wao mbali

Ni jambo nzuri sana kuwa katika mahusiano mema mkiwa wawili ili mzazi mmoja asiweze kuwaambia wanawe jambo mbaya kuhusu mzazi huyo mwingine." Mzee Juma aliongea.

Msanii Diamond atatulia licha yake kuwa na baby mama zaidi ya wawili?