Mudavadi asema ni afueni kwa wanafunzi maskini shule kufunguliwa mwakani

9-kenya4531-students(1)
9-kenya4531-students(1)
Ni afueni kwa wazazi wengi na wanafunzi baada ya serilali kutoa ratba kamili kuhusu mwaka huu wa akademia. Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi siku ya Jumatano alisema kwamba tangazo la Waziri wa elimu George Magoha lilikuwa habari njema kwa wazazi kuhusu mwelekeo wa sekta ya elimu nchini.

Soma pia;

Mudavadi vile vile alisema kwamba hatua ya kufutiliwa mbali kwa mwaka huu wa akademia ni afuani kubwa kwa wanafunzi kutoka familia maskini ambao kwa sababu ya hali yao ya uchochole hawawezi kupata masomo kwa njia ya dijitali. Alisema kwamba huku wanafunzi kutoka familia zinazojiweza wakiendelea na masomo kwa njia ya dijitali wenzao kutoka familia fukara wamesalia nyumbani bila masomo, hatua ambayo ingewaathiri sana ikiwa wizara elimu ingesisitiza mithihani ya kitaifa ifanyike kama ilivyokuwa imeratibiwa.

"Ili tusiwe na wale ambao wana advantage ya kuwa na online na kuna wale ambao hawana advantage ya kuwa na masomo ya online, lakini wote wanaletwa kufanya mtihani mmoja, huyu amesoma na huyu hajasoma, huo si ungwana," Mudavadi alisema.

Waziri wa elimu alitangaza kufutiliwa mbali kwa mwaka huu wa akademia na kusema kwamba shule zote zitafunguliwa Januari mwakani, wakati anatarajia kwamba maambukizi ya virusi vya corona yatakuwa yamedhibitiwa.  Waziri pia aitangaza kuwamba wanafunzi wote watarejelea madarasa na kuanza upya mwaka wa akademia.

Soma pia;

Mudavadi alipongeza hatua hiyo ya serikali akisema kwamba tangazo hilo la serikali litawapa wadau wote katika sekta ya elimu nafasi kupanga mikakati yao tayari kwa ufunguzi wa shule Januari mwaka ujao. Alisema wazazi na wanafunzi walikuwa wameachwa gizani kuhusu ni lini shule zingefunguliwa.

Kinara huyo wa ANC hata hivyo aliitaka wizara ya elimu kutoa muongoza mahsusi kubaini vile serikali itatekeleza mpangilio wa watahiniwa wa mitihani ya kitaifa kurejea shuleni huku wakizingatia kanuni zote za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Alitaka idara husika kueleza vile masharti kama ya kukaa umbali wa mita moja, usafi, kuvalia maski na mengineo yatazingatiwa shuleni.

Soma pia;

Pia ametaka idara husika kueleza taratibu ambazo zitafuatwa ikiwa kwa bahati mbaya mwanafunzi katika shule apatikana na vurusi hivyo. Ametaka serikali kuweka mikakati mahsusi itakayo hakikisha kwamba maisha ya wanafunzi, walimu na wafanyikazi wengine katika taasisi za elimu yanazingatiwa kabla ya shughuli za masomo kurejelewa.