Murenga, mfanyikazi wa zamani wa serikali alikuwa mwenyekiti wa Chancery Wright Insurance Brokers,aliaga dunia jumane asubuhi
Amemuacha mjane Magda Mugenda watoto wanne na wajukuu 10 pamoja na kitukuu mmoja .
Katika ujumbe kwa familia ya Murenga rais Kenyatta amemtaja mwendazake kama mtumishi wa serikali aliyekuwa na bidii na aliyefaulu kutoka utumishi wa umma hadi sekta ya kibinafasi kwa njia iliyowapa wengi matumaini katika biashara na waliotaka kumuiga .
Rais pia alikitaja kitabu cha marehemu Destined to Leave A Legacy, kama raslimali kubwa sana kwa vizazi vijavyo vya wafanyibiashara .
Marehemu alisomea Nyeri High School, Makerere University na Oxford University.
Akiwa Makerere University, Murenga alikuwa mwanafunzi wa rais mstaafu Mwai Kibaki na badaye wakawa washirika katika biashara .