Kila mwaka waislamu husherehekea Idd Hiyo ya kuchinja mfugo pamoja na familia ,marafiki na jamii baada ya salah ya alfajiri na kisha baadaye kuwagawa watu chakula na misada mingine kwa wanaoihitaji .
Hata hivyo mwaka huu kwa ajili ya janga la corona wengi wamelazimika kubadilisha jinsi wanavyosherhekea Idd kwani serikali hairuhusu wtau wengi kungomana katika sehemu moja.Salah ya Idd katika maeneo mengi imefanyika kwenye viwanja na maeneo ya wazi
Idd-ul-Adhais huadhimishwa kila siku ya 10 ya mwezi wa Dhul Hijja ,wa mwisho katika kalenda ya mwezi wa kiislamu kwa salaha ya asubuhi ,kuchinja mfugo -hasa kondoo kama kumbukumbu wakati nabii Ibrahim na mwanawe Ismael .
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi mbali mbali alhamisi walituma jumbe za kuwatakia waislamu Idd njema .