Afande Msanii! Samido aeleza jinsi anavyochanganya kuwa polisi na mwanamuziki

Mwanamuziki wa nyimbo za kikuyu Samido amekuwa na  mengi ya kusimulia kuhusu safari yake katika sanaa , Mwanamuziki huyo pia ni afisa wa polisi  na hilo halijamkosesha   fursa ya  kuendeleza  talanta  yake katika muziki .

Samido akizungumza na Massawe Jappani  amesimulia jinsi  alivyoteseka  utotoni na majirani walimsaidia kusoma kwa kumlipia karo  . Alianza kuimba mwaka wa 2009 akimsaidia mwanamuziki  Kamande wa Kioi

Kuhusu kali yake ya polisi anasema ;

"Kitengo cha polisi ni kama tumbo la mama. Tumbo la mama linaweza kuzaa, pasta na watu wengine. Watoto wote hawawezi kuwa sawa au kufanana..."

Samido anasema  wakati alipopata kazi ya polisi  alikuwa hana shati na hawezi kuiacha .

"Kazi ya polisi niliitafuta bila shati. Nilikuwa ninapitia shida sana na ilikuwa kama kivukio kwangu..."

Ameongeza kusema ;

"Changamoto kubwa katika maisha yangu kwenye familia, muziki, na kazi yangu kama afisa wa polisi ni muda..."