Msanii Willy Paul atumia maneno machafu kushtumu MCSK na baadhi ya wasanii

Saa chache baada ya msanii Willy Paul kudai kuwa pesa za wasanii ziimeliwa kupitia video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa instagram, hii leo ametumia maneno machafu kuwashtumu baadhi ya wasanii ambao hawajitetea na pia MCSK.

Huku kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram Willy alidai kuwa huwa anafanya kazi yake kwa bidii ilhali mtu anakuja kula pesa zake.

"Hivi ndivyo nafanya bidii ilhali makalio ambayo haina adabu inakuja kuniibia, lakini kwa nini serikali inakubali haya kutendekea?tuna ushahidi na huko hapa nje na hamna kitu ambacho kimefanyika 

Ni jambo la huzuni." Aliandika Willy Paul.

https://www.instagram.com/p/CE_BwU8n3_9/

Ni jambo ambalo limemgadhabisha msanii huyo huku akiwaibisha wasanii ambao hawateti kwa ajili ya haki zao huku akusema kuwa hivyo ndivyo watakuwa maskini kwa kukimya kwao.

"Aibu kwa wasanii ambao wamenyamaza wakigonja wapiganiwe na wengine , hivo ndio mtangeuzwa kuwa maskini na bibi zenu mpigiwe kuni na hawa watu

ni wakati umefika, tuje pampja tupigane kwa ajili ya jambo hili mara moja, mtaitwa maskini hadi lini?wacheni ujinga In the mean time x Avril iko hapo juu pia washaanza kuimezea mate hawa wezi FOOLS!"