Mshukiwa wa mauaji ya Kevin Omwenga Chris Obure alazwa hospitalini kabla ya kwenda kortini

obure-1
obure-1
Mfanyibiashara Chris Obure amelazwa hospitalini baada ya kusema kwamba  ni mgonjwa .

Hilo linafika kabla ya kufikishwa kwake kortini leo  ambapo mahakama inafaa kutoa uamuzi kuhusu ombi lake la kutaka kuachiliwa kwa dhamana .

Upande wa mashtaka unapinga kuachiliwa kwake kwa dhamana ukidai kwamba hatua hiyo itavuruga uchunguzi dhidi yake .

Obure  pamoja  na mlinzi wake Robert Bodo  wanakabiliwa na mashtaka ya kumuua  Kevon Omwenga .Siku ya alhamisi walishtakiwa pia kwa kutoiweka ifaavyo bunduki . Bunduki hiyo ndio iliyotumika katika mauaji ya Omwenga