Utafiti uliofanywa na Infortrak na kutolewa siku ya jumapili umeonyesha kwamba Milemba alishikilia nafasi ya kwanza kwa asilimia 75.4
Utafiti huo ulilenga kujua jinsi watu wa maeneo bunge walivyowaorodhesha wabunge wao ,maseneta ,waakilishi wa akina mama,MCA na magavana kati ya novemba/disemba mwaka jana hadi januari mwaka wa 2020.
Utafiti wa mwanzo ulifanywa kati ya agosti na septemba mwaka wa 2019
Jumla ya watu elfu 37,600 walihojiwa katika kaunti zote 47 .
Kulingana na utafiti huo Milemba anafutwa na , mbunge wa Emurua Dikiri Johana Ngeno katika nafasi ya pili kisha mbunge wa Mwala Vincent Musyoka ni wa tatu kwa asilimia 70.8
Wengine ni Christopher Aseka wa Khwisero kwa nafasi ya nne akiwa na asilimia 70 na Patrick Musimba wa Kibwezi West aliye na asilimia 69.8
Kulingana na utafiti huo mbunge wa , Isiolo South Abdi Koroputepo ndiye mwenye utendakazi duni Zaidi akiwa na asilimia 33.0
Mwingine katika nafasi ya pili kutoka chini ni Clement Muturi wa Kangema akifuatwa na Francis Kuria wa Molo
Mbunge wa Taveta Naomi Shaban anaongoza orodha ya wabunge bora wa kike akiwa na asilimia 61.6
Anafutwa na mbunge wa Kitui West MP Edith Nyenze akiwa na asilimia 58.4 mbunge wa Samburu West P Naisula Lesuuda akiwa na asilimia 57.5 ,Mary Njoroge wa maragwa akiwa na asilimia 56.8 na mbunge wa Malindi Aisha Jumwa akiwa na asilimia 53.3
Wakati huo huo mwakilishi wa akina mama wa KISUMU Rozah Buyu anaongoza orodha ya waakilishi wa akina mama wanaofanya vyema akiwa na asilimia 61.5
Anafuatwa na mwenzake nwa Homa bay Gladys Wanga kisha mwenzao wa Lamu Ruweida Mohamed ni wa tatu
Mwakilishi wa akina mama wa Kiambu' Gathoni Wamuchomba ndiye aliye na utendakazi duni sana akiwa na asilimia 39
Mwingine ni Janet Nangabo wa Trans Nzoia akifutwa na mwakilishi wa Nyamira Jerusha Mongina
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi, ambaye ni mtetezi mkubwa wa naibu wa rais William Ruto mbunge wa makadara George Aladwa na mbunge wa Nakuru Town west Samuel Arama ni miongoni mwa wajumbe ambao hawakusema lolote bungeni mwaka wa 2019
Wengine ambao hawakutamka lolote bungeni ni mbunge wa Shinyalu Justus Kizito, Alfred Sambu wa Webuye East na John Naicca wa Mumias West.